Na Mwandishi Wetu,Dar es Salaam
MAMLAKA ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) imesema jumla ya mashauri 1200 ya kesi za dawa za kulevya yalipekwa mahakamani ambapo kati ya hayo mashauri 990 sawa na asilimia 75 na kuwatia hatiani watu zaidi ya watu 1000 katika kesi zilizosikilizwa mwaka 2025.
Akizungumza katika semina ya wadau wa DCEA Kaimu Kamishna Msaidi wa Uratibu na Mashtaka wa Mamlaka hiyo Mfinanga Mselemu amesema kuwa katika kipindi cha mwaka 2025 kumefanyika operesheni mbalimbali za ukamataji ikiwemo kukamata wafanyabiashara nguli ambapo watu hao miongoni mwao walikutwa hatia na kupelekwa mahakamani.

“Kwa mwaka 2025 jumla ya mashauri 1200 ya kesi za dawa za kulevya yalipekwa mahakamani ambapo kati ya hayo mashauri 990 sawa na asilimia 75 na kuwatia hatiani watu zaidi ya watu 1000 ambapo watu hao wote walishughulikiwa kwa mujibu wa sheria zilizopo zinazopambana na dawa za kulevya ikiwemo kufungwa ,”amesema Kamishna Mselemu.
Amesema katika kundi hilo la watu waliotiwa hatiani pamoja na kufungwa pia wapo waliotaifishiwa mali zao ambazo wamezipata kutokana na biashara hiyo.

“Ni wakati wa jamii kufahamu sasa kuwa biashara hii hailipi,sisi ni wajibu wetu wakupambana na dawa za kulevya ili kuiokoa jamii ambayo kwa kiasi kikubwa wamekuwa wakiangamia kutokana na dawa hizi,”amesema Kamishna Msaidizi Mselemu.


