Na.Mwamdishi Wetu,Dodoma
Mkurugenzi wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), Ramadhani Kailima, leo Novemba 4, 2026, ametembelea na kukagua vituo vya kupigia kura katika Jimbo la Chamwino, mkoani Dodoma, ili kujionea mwenendo wa maandalizi na utekelezaji wa zoezi la upigaji kura.
Akiwa katika ziara hiyo, Kailima ameridhishwa na maandalizi ya zoezi hilo na kuwataka wasimamizi wa vituo vya kupigia kura kuhakikisha wanatoa ushirikiano unaostahili kwa mawakala wa vyama vya siasa pamoja na wananchi wanaojitokeza kutekeleza haki yao ya kidemokrasia ya kupiga kura.

Uchaguzi huo unafanyika sambamba na Uchaguzi Mdogo wa Madiwani katika kata 11 za Tanzania Bara.
Kata hizo ni Nonde iliyopo Halmashauri ya Jiji la Mbeya; Lugenge, Halmashauri ya Mji Njombe; Bargish, Halmashauri ya Mji Mbulu; Makole, Halmashauri ya Wilaya ya Muheza; Mwera, Halmashauri ya Wilaya ya Pangani; na Oldonyosambu, Halmashauri ya Wilaya ya Ngorongoro.

Kata nyingine ni Igalula iliyopo Halmashauri ya Wilaya ya Uyui; Shelui, Halmashauri ya Wilaya ya Iramba; Mvumi, Halmashauri ya Wilaya ya Kilosa; Nyarero, Halmashauri ya Wilaya ya Tarime; na Ilolangulu, Halmashauri ya Wilaya ya Mbogwe.



