MWEKEZAJI TOTAL ENERGIES AWATAKA WATANZANIA WALIOPO NJE KUJA KUWEKEZA NCHINI

Na Mwandishi Wetu,Dar es Salaam

WAFANYABIASHARA wa Tanzania wanaoishi nchi za nje wametakiwa kurudi nchini na kufanya uwekezaji  ili  kuchangia kuinua uchumi na kuendeleza Taifa kwa ujumla.

Kauli hiyo imetolewa leo Oktoba 6, 2025 na Mmiliki wa kituo cha mafuta cha Total Energies kilichopo Kimara Godfrey Nyashage wakati akizindua kituo hicho ambacho ni kipya.

Alisema yeye ni mmojawapo wa wawekezaji waliowekeza nje ya nchi ambapo anafanya biashara za vituo vya mafuta nchini Congo.

Alisema ni wakati wa Watanzania wanaoishi nje kurudi nyumbani na kufanya uwekezaji kwakuwa itasaidia kuwasaidia watanzania kupata ajira na kuongeza mzunguko wa  fedha nchini.

“Diaspora nili vizuri waje kuwekeza nyumbani uchumi wetu tunatakiwa kuujenga wenyewe tusitegemee mtu kutoka nje,hivyo ni vema tuje kuwekeza nchini na kuinua uchumi wa Tanzania”alisema Nyashage.

Alisema kuwa alianza kuwekeza Congo ambapo amefanya biashara kwa miaka kumi na mpaka sasa ana  vituo zaidi ya kumi vya mafuta.

“Baada ya kuwekeza kule niliona nianze kurudi nyumbani,nikatafuta eneo hapa nikaangalia nifanye na nani biashara hii  nikaona nifanye na Total kwa sababu mafuta yao ni mazuri,”alisema Nyashage.

Alisema ufunguzi wa kituo hicho ni mwanzo tu ambapo ameeleza kuwa lengo lake ni kuhakikisha ndani ya miaka miwili au mitatu awe na   vituo vitatu vinne.

Alisema mpaka sasa kituo hicho kimeshatoa ajira kwa watu 26 katika vitengo mbalimbali.

Naye Meneja wa Maendeleo ya Biashaara wa kampuni  Total Energies Jane Mwita alisema kituo hicho kimejengwa kupitia Programu  Dodo ambapo kampuni  Total energy wanaingia ubia na wafanyabiashara binafsi wenye biashara  kwa ajili yakujenga vituo vya mafuta kulingana na vigezo vilivyowekwa.

“Lengo la programu hii ni kuwainua wafanyabiashara wa mafuta kwakuwa kampuni hiyo inajulikana hivyo inawasaidia kupata wateja, wafanyabiashara ambao wanajihusisha na mafuta wakitumia majina yao hawawezi kukua tofauti wakitumia jina la Total.

Tukifanya ubia na total  biashara zinakua,lakini ukiwa na ubia na total kituo kitaweza kuuza lita laki mbili na nusu au tatu,”alisema Mwita.

Naye Juma Mohamed ambaye ni Katibu wa Umoja wa Madereva Bajaji kwa Msuguri alisema uwekezaji huo umewafurahisha,umewarahisisha upatikanaji wa mafuta.

“Sisi inaturahisishia  katika ufanyaji wetu wa kaziWawekezaji wametambua kuwa sisi ni shemu ya kufikiwa tumeweza kupata kituo karibu,mara ya kwanza tulikuwa tunaemda Mbezi tukafikia hatua tunavuka barabara lakini sasa tunaweka hapa karibu bila shida ya aina yoyote hata madereva wa Kirikuu wanaweka mafuta hapa,”alisema Mohamed.

Ufunguzi wa kituo hicho umefanya kampuni ya Total Energies kuwa na vituo 25 vya ubia vinavyojishughulisha na uuzaji wa mafuta,gesi za majumbani vilainishi,maduka ya makubwa lengo ni kuhakikisha wateja wanapofika vituoni hapo wanapata huduma zote.