OMO AWATAKA WAZANZIBAR KUSHIKAMANA KUMPIGIA KURA AWABORESHEE MAISHA

Na Mwandishi Wetu,Zanzibar

MGOMBEA Urais wa Zanzibar kupitia Chama cha ACT Wazalendo, Othman Masoud Othman, amewataka Wazanzibari wote kushikamana kwa pamoja na kumpigia kura katika Uchaguzi Mkuu ujao ili kuinua maisha ya wananchi na kuinusuru Zanzibar.

Akizungumza katika mkutano wa kampeni uliofanyika Shumba ya Vyamboni, Jimbo la Tumbe, Mkoa wa Kaskazini Pemba, Othman alisema kuwa ni wakati sasa wa Wazanzibari kuungana bila kujali tofauti za vyama vyao vya siasa, bali kuangalia mustakabali wa nchi yao.

Zanzibar tunaiokoa kwa umoja wetu. Tusiangalie vyama, tuangalie nani ana maono ya kweli ya kuleta mabadiliko na kuinusuru nchi yetu,” alisema Othman

Alisisitiza kuwa ACT Wazalendo ndicho chama kinachoongoza kwa dira, maono na mipango ya maendeleo itakayowezesha Zanzibar kuwa na uchumi imara, ajira kwa vijana na huduma bora kwa wananchi wote