ULEGA:TUMUOMBEE RAIS SAMIA APATE NGUVU YAKUENDELEA KUTUONGOZA

Na Aziza Masoud,Dar es Salaam

WATANZANIA wametakiwa kuendelee kumuombea dua Rais Dk.Samia Suluhu Hassan ili aendelee kupata nguvu kufanya mambo makubwa  ya maendeleo nchini na kwamba wanapaswa kuhakikisha anapata uhakika wakuendelea kuongozo nchi kupitia uchaguzi mkuu ujao wa mwaka 2025.

Kauli hiyo imetolewa jana usiku Desemba 14,2024 na Mbunge wa Mkuranga Abdalla Ulega katika hafla ya sherehe ya Maulid ya kumtukuza Mtume Mohamad (S.W) iliyoandaliwa na Baraza la Waislam Tanzania (Bakwata) mkoa wa Pwani  ambazo hufanyika kila mwaka.

Ulega mabye pia ni Waziri wa Ujenzi alisema Dk. Samia  anafanya kazi kubwa ya kuifungua na kuleta maendeleo nchini hivyo ni jukumu la wananchi kuhakikisha wanamuombea dua aweze kuendelea kuongoza kwa busara.

“Rais  Samia amefanya kazi kubwa sana,kama ni kwenyw mpira mpaka sasa kwa sisi  ambaye ni wasaidizi tulio chini yake tunasema kwa pamoja tunaongoza kwa goli tatu,sasa tuongeze mengine ili ikifika 2025 raisi awe ashafunga magoli yake sita au saba awe mshindi hii ni kwa sababu kafanya kazi kubwa sana,”alisema Ulega.

Alisema wakazi wa  wilaya ya Mkuranga wanapaswa kumshukuru rais Samia kwa sababu pamoja na maboresho mengi yanayoendelea amefanya jambo la muhimu kwakumteua kuwa Waziri wa Ujenzi ambapo itamsaidia kusimamia kuzipa hadhi na kuzifanyia maboresho barabara za eneo hilo.

“Kumekuwa ba maboresho ya barabara kila mwaka ambapo mpango ni kupandishwa hadhi barabara kutoka Msanga,Kusarawe kutokea Kitonga kuna barabara ya Vikindu,Vianzi Sambatini mpaka kutoka Kigamboni zote ziliapaswa kupandishwa hadhi sasa mpandisha hadhi ndiyo miye ndo maana nawaambia tutumie hadhira  hii kumshukuru Mungu na tumuombee dua nyingi sana RaisDk.Samia,”alisema Ulega.

Akizungumzia kuhusu barabara za Kisemvule  Mwandege  ambazo miji yake ni mikubwa lakini kuna taa chache hivyo aliahidi kutekeleza suala hilo kupitia wizara ya Ujenzi.

“Si barabara za Mkuranga tu  namuahidi Rais Samia kumsaidia kufanya kazi nchi nzima  usiku na mchana,Magharibi na Mashariki,Kaskani na Kuusini,”alisema Ulega.

Akizungumzia kuhusu foleni ya Mbagala Ulega alisema “Mashehe niseme kuwa Mungu anatuthibitishia kila hatua yetu ya kwamba unapomuomba  atakujibu,mimi ni mwrnye kilio kikubwa sana kwa mambo ya barabara na  kama lipo jambo linatusumbua ukiacha ya vijijini mwetu ambapo kote kunataka maboresho ambapo baadhi wakandarasi wapo kazini na maboresho mengine yanataka kuanza, kitu ambacho ni usumbufu mkubwa ni foleni ya Mbagala

“Hii inasababisha  watu Dar es Salaam wanapokuja huku tunawaambia ondokeni saa nane isizidi saa tisa yaani watumie masaa matatu kwa hofu ya kipande cha Kongowe kuja huku,kuna pale Rangi Tatu na Mzinga mpaka ufike Kongowe unaweza ukatoka Kisiju vizuri mno,unaweza ukatoka Mkamba vizuri mno ukifika mahala pale unakwama.

“Nilivyopokeea wizarani nikawaambia wenzangu yaani hakuna kitu kimenifurahisha  na kujibu sala zangu nikikumbuka kadhia ya Mbagala  kwa kweli nakwenda kuanza nayo mengine sijayataja  lakini tuombe dua tuhakikishe tunakimbizana na  ili mambo yetu yaende vizuri,”alisena Ulega.

Katika ghafla hiyo Ulega pia aliwatangazia viongozi wa Bakwata kuwakabidhi gari kwa ajili ya ofisi ya wilaya  pamoja na pikipiki katika kata zote 25.

Awali  Shehe wa mkoa wa Pwani Hamis Mtupa wakati akitoa mada ya maadili na kudumisha amani aliwataka watanzania  kulinda amani iliyopo nchini.

Tulindw  amani sisi tunaishi hapa kwa sababu ya Amani iliyopo wapo watu wanasema wamepata tu Uhuru wa bendera kwamba nchi haina uhuru hao watu hawapaswi kupewa madaraka watakuja kuvuruga Amani,”alisema.

Naye Mkuuu wa wilaya ya  Mkuramga Khadija Nassir Alli alisema serikali inawategemea  sana viongozi wa dini katika kuonyesha  njia lakini pia katika kuwaongoza  namna gani nzuri kuongoza nchi  hususani katika  wilaya ua Mkuranga.

Alisema viongozi wa dini wamekuwa wakionyesha  njia yakuyafikia maendeleo ya nchi kwakuzingatia  Amani.

“Hivi karibuni tumetoka  kwenye uchaguzi tunawashukuru  viongozi wa dini kwakutuongoza vema katika tukio hili muhimu na mimi ndo ulikuwa uchaguzi wangu wa kwanza bila nyinyi nisingeweza kufanikiwa vizuri asanteni sana viongozi wangu na wazee wangu,”amesema Khadija.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *