Wananchi watakiwa kutembelea banda la GCLA Sabasaba

Na Mwandishi Wetu,Dar es Salaam

MWAKILISHI  wa Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali (GCLA) Stafford Maugo, amewataka wananchi wa kitembelea banda lao katika Maonesho ya 48 ya Kimataifa ya Biashara (Sabasaba) kujionea shughuli mbalimbali wanazofanya ili waweze na kujifunza kuhusu masuala ya kemikali.

Amesema kupitia maonesho hayo watawaelezea aina ya chunguzi wanazofanya kwa kushirikiana na taasisi binafsi na serikali.

Ameyasema hayo jana jijini Dar es Salaam katika maonesho hayo.

“Mfano polisi akikamata dawa za kulevya, bangi na mirungi atazileta hapa kwenye maabara ya rufaa kwaajili ya kufanya uhakiki kama ni kweli ni dawa za kulevya au kitu kingine.

Maugo ambaye pia ni mkaguzi wa kemikali amesema pia kesi za ubakaji askari wanakamata vielelezo na kuvipeleka kwenye maabara ili kumfahamu muhusika.

Amesema pia kuna huduma za vinasaba wapima ili kutatua migogoro ya familia kuhusu uhalali wawatoto.

Maugo amesema pia wanachunguza kuhusu jinsi tata kwa watoto waliozaliwa na jinsia mbili lengo ni kusaidia madaktari kutambua jinsi iliyotawala.

“Vipimo hivyo vitamsaidia daktari kuondoa ile jinsi ambayo haijatawala,” amesema Maugo.

Amesema katika maonesho hayo wanawasaidia wateja wa kemikali kujisajili na kuingia kwenye mfumo wa maalum wa huduma za kemikali.

Amesema wadau wote wa kemikali  wanatakiwa kujisaili ili waweze kuunganishwa

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *