MIAKA MINNE YAKUTEKEZA MTANDAO WA DAWA ZA KULEVYA NCHINI

DCEA YAELEZA JINSI ILIVYOVUNJA MITANDAO MIKUBWA YA DAWA MITANO

Na Aziza Masoud,Dar es Salaam

SERIKALI ya Awamu ya sita imetimiza miaka minne madarakani tangu Rais Dk. Samia Suluhu Hassan alipoingia madarakani Machi 19 mwaka 2021 baada ya kifo cha Rais wa Awamu ya Tano Dk.John Magufuli.

Tangu aliposhika wadhifa huo Dk.Samia amekuwa akifanya maboresho na kuimarisha taasisi na idara na taasisi mbalimbali za serikali ili kuweza kutoa huduma bora na zinazokidhi Watanzania.

Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya nchini (DCEA) ni miongoni mwa taasisi iliyofanyiwa maboresho makubwa katika kipindi hiki cha miaka minne ambapo mapambano dhidi ya biashara hiyo haramu yamekua kwa kasi.

Akizungumza katika mahojiano maalum na waandishi wa habari Kamishna Jenerali wa DCEA Aretas Lyimo katika kipindi cha miaka minne ya  serikali ya awamu ya sita  mamkala imejikita kiasi kikubwa katika kudhibiti na kuteketeza mtandao dawa za kulevya ambavyo mpaka sasa wamevunja mitandao mitano ya dawa za kulevya iliyokuwa ikiongozwa na wafanyabiashara  wakubwa kutoka mikoa mbalimbali.

“Zamani kulikuwa na watu wanaitwa mazungu ya unga ilikuwa hata ukitoa taarifa kuhusu hawa watu na wewe unakuwa matatani, maisha yako yanakuwa hatarini lakini sasa hivi hao watu hawapo hii ni mafanikio ya awamu ya sita .

“Kulikuwa na watuhumiwa wakubwa ambao hawashikiki kwa mara ya kwanza umesikia watu wakubwa wanakamatwa na mizigo mikubwa Mfano yupo mmoja tumemkamata na kilo 3500 tulikamata Disemba 2023 ni kiasi kikubwa hakijawahi kukamatwa tangu Tanzania iumbwe ,hii ni mafanikio ya awamu ya sita,”amesema Kamishna Lyimo.

Amesema  mapambano haya pia yanachagwiza zaidi kutokana na rais kuwa  mwanamke hivyo hakuna mama  anayependa   watoto wake waharibike na amekuwa akitoa msisitizo mkubwa katika kipindi cha uongozi wake

 Amesema mpaka sasa DCEA imeshaua mitandao mitano ya usafirishaji na usambazaji wa dawa za kulevya ambayo ilikuwa hatari nchini  ambapo miongoni mwa viongozi wa mitandao hiyo watatu ni Watanzania huku wawili wakitokea nchi za Nigeria na Pakistan 

“Mtandao huu ulikuwa ukisambaza dawa za kulevya aina ya cokaine,tangu wakamatwe watu hawa usambazaji wa dawa hiyo kwa sasa umepungua,tunajua haziwezi kuisha kabisa ndo maana tunasema haya ni mapambano,”amesema Kamishna Lyimo.

Amesema awali Tanzania ilikuwa ndo lango la kupitisha dawa za kulevya  ambapo mtu akiingia nchi yoyote akisema ametoka Tanzania lazima awekwe pembeni kwa ajili ya ukaguzi zaidi.

“Zamani  ukienda nchi za watu ukionyeshqa passport (hati ya kusafiria) ya Tanzania lazima uwekwe pembeni,watu walikuwa wanakamatwa katika nchi mbalimbali kila wiki lazima usikie kuna mtanzania kakamtwa ama kanyongwa hii ni kutokana na ilikuwa lango lakini ukamataji wa wafanyabiashara hawa wakubwa umeondoa hali hiyo,”amesema Kamishna Lyimo.

Uanzishwaji wa Kanda na Mafanikio yake

Amesema katika kuhakikisha wanaendeleza udhibiti na mtandao wa dawa za kulevya mamlaka imeanzisha Kanda tano ambazo awali hazikuwepo na kwamba watu wote wanatoka makao makuu kwenda mikoani kufanya shughuli zakupambana na dawa za kulevya na kufanya ofisi hiyo kutumia fedha nyingi.

Amesema kanda zilizoanzishwa ni pamoja na Kanda ya  Kaskazini ambayo inajumlisha mikoa ya  Manyara,Arusha Tanga kwa ajili ya kudhibiti mipaka.

‘Kanda ya Arusha imeleta mafanikio makubwa kwakuwa mikoa hiyo ilikuwa inaongozwa kwa kilimo cha bangi.

“Kutokana na operesheni nyingi watu wamegundua wanaanza kulima bangi ndani ya nyumba  wanalima kwenye makopo hata hawa nao sasa tumewagundua na tumeanza kuwakamata,”amesema Kamishna Lyimo.

Amesema kutokana na kasi ya ulimaji bangi katika mikoa ya Arusha kulikuwa kasi kubwa la ongezeko la waharifu lakini tangu kuanzishwa  kwa Kanda hiyo hata takwimu za uharifu zimepungua. 

Amesema kanda nyingine ni Kanda ya  Ziwa  ambayo inajumlish mikoa ya Mwanza,Kagera,Geita,Mara,Shinyanga.

Amesema katika mkoa wa Mwanza hali ya matumizi ya dawa za kulevya hasa heroin ilikuwa juu lakini  kwa sasa imepungua.

“Zamani walikuwa watumiaji wa dawa za kulevya unawakuta tu hasa kwenye maeneo ya ziwa lakini tangu kuanzishwa kwa Kanda hiyo kumekuwa na operesheni kubwa.

 “Pia  operesheni za mkoa wa Mara zimeleta mafanikio zamani watu walikuwa hawasogei wakienda walikuwa wanavamiwa wanawapiga wanajeruhiwa lakini baada ya mamlaka kuanzisha Ofisi kule tuliwabaini wakorofi wanaolima bangi tukawakamata,kwa sasa wanakimbilia katika mto Mara huko  hilo eneo ni mbali sana unaenda na gari unazunguka zaidi ya masaa mawili hekari  tatu huko wananchi walikuwa wametawala lile eneo kama hakuna serikali sasa hivi tumelidhibiti,”amesema Kamishna Lyimo.

Ametaja Kanda nyingine ni Kanda ya  ya kati ambayo inajumlisha Dodoma,Singida,Tabora na Kigoma ambapo lengo ni kuhakikisha makao  makuu ya nchi hakuna uharifu Kwa sababu asilimia 99 wanafanya uhalifu ni watu wanaotumia dawa za kulevya.

“Wengi wanaofanya uhalifu tuliowakata hata wale Panya road wa Dar es Salaam asilimia 99 wanatumia bangi,bangi inaleta ujasiri sana na kuharibu uwezo wakufanya maamuzi kama binadamu na kuamua kufanya uharifu,”amesema Kamishna Lyimo.

Amesema katika kanda hiyo mkoani Dodoma  alikamatwa  tulikamata zungu la unga ambaye alikuwa anauza unga kw watu wote wa mkoa huo.

“Huyu kulikuwa hakuna mtu aliyekuwa anaweza  kumkamata mbaya zaidi wauza unga ni wafadhili wakubwa katika siasa,dini na mambo mengine yakijamii ili kuhakikisha akikamatwa watu wengi wanapiga kelele hivyo kama hujajipanga kwakumkamata na vidhibiti unamuachia.

“Awamu hii ndo maana mtu akikamatwa na dawa za kulevya hakuna msamaha na kila tunayemkamata ushahidi upo na ndo maana tunawakamata na kiwango kikubwa ili usije kusema sio zako,”

Amesema kupitia operesheni za Kanda hiyo pia wamekamata shamba la bangi la hekari 14 wilayani Chamwino.

“Katika hali ya kawaida mtu asingeweza kuwaza kama kuna mtu anaweza kulima bangi katika ya jiji eneo kama Chamwino watu walikuwa wanajiamini sana,lakini sio hilo tu hata wale walimaji walikuwa na silaha za moto,”amesema Kamishna Lyimo.

Amesema mbali na hilo wilaya ya Kondoa pia wameteketeza hekari 335 na bado operesheni zinaendelea kwakuwa katika hali ya kawaida hakuna mtu angewaza kuwa  Dodoma wanalima bangi na tunafanya hivyo kwakuwa sisi tunaenda kwenye chanzo cha tatizo  usipofanya hivyo utajikuta bangi zinaingua tu hujui zinatoka wapi.

“Tukifanya tu operesheni za mitaani unakamata wavutaji na wasambazaji kila siku bangi zitakuwa zinaingia,”amesema Kamishna Lyimo.

Amesema pia katika mikoa ya Singida na Tabora operesheni kubwa zimefanyika kwenye misitu.

Ametaja Kanda nyingine  kanda ya Pwani Lindi Mtwara Ruvuma na Pwani yenyewe ambapo operesheni inaendelea kulinda mipaka na kuhakikisha hakuna dawa  inaingia.

Amesema pia kuna Kanda ya juu Kusini Rukwa,Mbeya ambapo mamlaka  imeimarisha intelijensia ndani ya Kanda mzima.

Amesema kali ya ulimaji wa  bangi umepungua lakini kumekuwa na bangi mpya aina ya skanka ambayo inatumika zaidi nchini ni kali ina madhara makubwa.

Akizungumzia kuhusu adhabu zinazotolewa kwa wafanyabiashara hawa kwa mujibu wa Sheria amesema wanakamatwa na dawa za viwandani za kulevya kuanzia gramu 200 haina dhamana na kifungo chake kinaanzia miaka 30 na wanaokamatwa na dawa za kulevya kuanzIa gramu 500 adhabu yake kifungo cha maisha.

Kwa upande wa mirungi amesema wanaokamatwa na  kuanzia kilo 20 haina dhamana kifungo chake miaka 30 kuanzia kilo 100 kifungo cha maisha na hii inatokana na  kuimirishwa Kwa Sheria.

*Ununuzi wa vifaa na mafunzo*

Amesema serikali ya awamu ya sita imekuwa ikinunua gari za gari za operesheni kupitia rasilimali fedha pamoja na kuongeza watumishi 

“Kwa sasa tunaweza kufanya operesheni Tanzania nzima awali mamlaka ilikuwa na watu 102 sasa wameongezeka,pia mamlaka imeongeza kutoa mafunzo tunapata mialiko katika nchi mbalimbali kama Singapore,Viena,Marekani hii inatokana na uhusiano inapata mafunzo na kuwa na weledi,”amesema.

Amesema pia kwa mara ya kwanza mwaka 2023 wamejenga maabara imekamilika 2024 na itaanza kutumika mwaka huu.

Amesema maabara itakuwa  na vifaa vya kisasa ambacho kimoja kinauzwa karibu Milioni 200.

“Vifaa hivyo unapima dawa zaidi ya sekunde mbili unajua dawa gani na kingine kina uwezo wakupima dawa zaidi ya 1200 kwa wakati mmoja,kuna kifaa kingine sio lazima utoe kifurushi upime kama kina dawa bali unagusisha tu hiyo   inasaidia kutokufungua vitu vya watu ambavyo vinafungwa,lengo ni kujengwa mahusinao mazuri kati ya wananchi mashirika mbalimbali Kwa sababu zamani ilikuwa unamuweka mtu uwanja wa ndege unamchelewesha kumbe sio dawa watu walikuwa wanaona kama usumbufu,”amesema Kamishna Lyimo.

Elimu ya dawa za kulevya

Amesema Rais Dk.Samia ameimariaha eneo la operesheni lakini pia tunatoa elimu kwa jamii ili watu waelewe kuhusu dawa za kulevya.

“Mpaka sasa tumefikia watu 28,000,000 ambayo ni sawa na nusu ya watanzania  sasa hivi watanzania wengi wanajua madhara ya hizi dawa na tunatengeneza vipeperushi vyakutosha tumeshanunua mtambo wakutemgeneza vipeperushi,”amesema.

Amesema pia wameanzisha vilabu vyakuelimisha mashuleni ambapo zipo pamoja na klabu za Takukuru inaitwa yakupinga rushwa na dawa za kulevya.

Matibabu

Amesema serikali imeanzisha vituo  mbalimbali zakutibu walaibu ambapo awali vilikuwa 11,sasa hivi vimefika 16  vinahudumua waraibu18,0170.

Amesema pia vituo vitano vinajengwa viwili vimekamilika vinasubiri mashine za kisasa zimeshaagizwa.

Amesema pia vituo vitatu vimeanza kujengwa katika maeneo ya Mkuranga Kilimanjaro Kahama.

“Mafanikio makubwa ya awamu ya sita kujengwa uchumi endelevu watu wakiwa na afya hivyo lazima kuongeza mapambano ya dawa za kulevya,kuna nchi moja tulienda ukifika mtaani ni  waraibu tu wamejaa serikali ikitaka kuajiri watu wanachukua kutoka nchi nyingine wanapewa uraia,”amesema Kamishna Lyimo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *