COPRA YAGAWA MBEGU ZA MBAAZI KWA WAKULIMA DODOMA
Na Asha Mwakyonde, Dodoma MAMLAKA ya Udhibiti wa Nafaka na Mazao Mchanganyiko (COPRA) leo imekabidhi tani 2.5 za mbegu za mbaazi kwa Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Rosemary Senyamule, kwa lengo la kuwanufaisha wakulima wa Halmashauri za Chemba, Kondoa na Kongwa wanaotumia mfumo wa Stakabadhi za Ghala kuuza mazao yao. Akizungumza Januari 6, 2025 jijini…

