Na Mwandishi Wetu,Dar es Salaam
IKIWA zimebaki siku mbili kabla yakuanza kwa Maonesho ya Biashara ya Kimataifa maarufu kama Sabasaba Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Albert Chalamila amewahakikishia wakazi wa Dar es Salaam usalama wakati wote wa maonesho ili kuwawezesha wakazi wa jiji hilo kufurahia maomesho hayo.
Akizungumza leo Juni 25, 2026 wakati alipotembelea kwa ajili ya kuangalia maandalizi ya maonesho hayo ambayo kwa mwaka huu yanatimikza miaka 50 ,Chalamila amesema ofisi ya mkuu wa mkoa kwakushirikiana na Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (Tantrade) wamejipanga kuhakikisha ulinzi na usalama unakuwa kwa kiwango cha juu katika eneo hilo na mkoa mzima.

“Tumejipanga vizuri kuhakikisha kwamba ulinzi na usalama katika maeneo haya unakuwa kwa kiwango ambacho hakijawahi kuonekana naomba,niwathibitishie ndugu waandishi wa habari hakuna mtu yeyote ambaye atahamasisha vurugu katika maonesho au ukanda wowote na akabaki kuwa salama vyombo vya dola pamoja kwa kushirikiana na wananchi,”alisema Chalamila.
Alisema wamejipanga kwa dhati kuhakikisha wanaendelea kulinda Taifa lisivamiwe na adui yoyote wa ndanj au nje ya taifa kwa kuwa maonyesho hayo ni kielelezo kikubwa cha utajiri, fahari na utamaduni wa mtanzania.

“Tutaendelea kuhamasisha wananchi wote moja waweze kushiriki lakini pia waweze kushiriki kwa kufanya biashara lakini na kuweza kushiriki kuilinda amani ya taifa kwa kukataa vurugu fujo,muonyeshe mtu yeyote ambaye hana nia nzuri ili tuweze kumbaini na vyombo vya dola viweze kushughulika naye,”alisema Chalamila.
Alisema ofisi ya mkuu wa mkoa imeandaa utaratibu mzuri kuhakikisha wananchi wanafika katika eneo hilo kwa urahisi iliwemo usafiri wa mwendokasi.

Alisema maonesho hayo yanaanza Juni 28 lakini tunategemea kwamba yatafunguliwa rasmi Julai tatu 2026 na kumalizika Julai 13 2026.
Alisema maonesho hayo mbali na kuhamasisha uchumi wa mtu mmoja mmoja lakini pia yanakuza pato la Taifa,kuhamishsa uchumi wa vikundi na kupunguza umaskini kwa wakazi wa Dar es Salaam.


