SABASABA YAJA KIDIGITALI ZAIDI


Na Mwandishi Wetu,Dar es Salaam

SERIKALI imesema imekamilisha maandalizi ya Maonesho ya 50 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (Sabasaba), kwa kuboresha miundombinu na kuanzisha mifumo ya kidijitali ya ununuzi wa tiketi na kuwaongoza wageni kufika katika mabanda mbalimbali, hatua inayolenga kuongeza ufanisi na kuondoa msongamano wa wananchi watakaotembelea maonesho hayo.

Akizungumza leo Juni 26, 2026 jijini Dar es Salaam Waziri wa Viwanda na Biashara, Judith Kapinga, alisema lengo la kuweka mfumo huo ni kuondoa usumbufu katika viingilio pamoja na kuwasaidia watembeleaji ndani ya maonesho hayo kujua ramani za maeneo wanayotaka kwenda ndani ya mabanda.

“Serikali imeweka wataalamu maalumu kwa kushirikiana na Mamlaka ya Serikali Mtandao (e-GA) kuhakikisha mifumo hiyo inaendelea kufanya kazi hata endapo kutatokea changamoto za kiufundi, huku wananchi ambao hawatakuwa wamenunua tiketi mapema wakipata huduma hiyo kidijitali wanapowasili viwanjani na wanapoenda kutafuta mabanda.

“Muonekano mpya wa maadhimisho ya Jubilee ya miaka 20 yamerahisishwa sana kama mnavyofahamu ile eneo ni kubwa naonyeshaji wako wengi kwa hiyo tumeweka njia za teknolojia za kurahisisha upatikanaji wa eneo ambalo mtu anataka kwenda kuwa tumeweka wifi ndani ambapo simu yako itaweza kukuongoza kwenda kwenye banda au kwenye biashara au kwenye lile eneo la onyesho “alisema Kapinga.

Alisema kutakuwa na aplikesheni inayoitwa Tantrade biashara up ambapo wenye simu za android wana uwezo wa kuingia kwenye aplikesheni ya country biashara up na kisha wakaanza kununua tiketi zao kuanzia sasa.

Alisema Ai amesema maonesho hayo yameendelea kuwa jukwaa muhimu la kukuza biashara na viwanda kwa kuwapa wazalishaji na wawekezaji fursa ya kutangaza bidhaa, kupata masoko mapya na kujifunza teknolojia za kisasa kutoka mataifa 23 yatakayoshiriki katika maonesho ya mwaka huu.

Kapinga ameongeza kuwa Wizara imeanzisha kituo maalumu cha Business Clinic kitakachotoa huduma za papo kwa papo kwa wafanyabiashara na wawekezaji wenye changamoto zinazohusu taasisi mbalimbali za biashara na uwekezaji, huku akiwahimiza Watanzania kutumia maonesho hayo kujifunza teknolojia mpya, kutafuta masoko na kutumia fursa zinazochochea ukuaji wa uchumi wa taifa.
Alisema kupitia Maonesho jumla ya ajira za 22,800 zitapatikana na kuwasaidia wananchi kuwainua kiuchumi.