TRA YAZINDUA OFISI YA WALIPA KODI WENYE HADHI YA JUU

Na Aziza Masoud,Dar es Salaam

MAMLAKA ya Mapato Nchini (TRA) imezindua Ofisi ya walipa kodi binafsi  wenye hadhi ya juu ambapo kwakuanza  wateja 158 wamekidhi vigezo vyakuhudumiwa wakiwemo wamiliki wa kampuni binafsi 111 zinazoingiza mapato ya Sh Bilioni 20 kwa mwaka.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa ofisi hiyo iliyopo katika jengo la Golden Jubilee Tower,Kamishna Mkuu wa  TRA, Yusuph Mwenda amesema  lengo la kufungua ofisi hiyo ni kuboresha huduma pamoja na kuwaomdolea usumbufu kundi hilo ambalo linaliingizia Taifa fedha nyingi.

“Huduma hiyo ya hadhi ya juu  inatolewa kwa wamiliki wa kampuni ambao wanaingiza Sh Bilioni 20 kwa mwaka,wamiliki wa hisa katika makampuni amazo zina thamani ya zaidi ya Sh bilioni 2.5,mtu mwenye ubia na kampuni zinaingiza faida Sh Bilioni 20  kwa mwaka.

“Wale wote waliopata fursa zakuletwa gapa niwapongeze,wateja 111 wapo na sifa zakukaa kwenye kodi za juu zaidi  na viongozi 47 nao wamo,nawahakikishia  huduma zitakuwa bora zonazoendana na hadhi zao lakini pia itaondoa usumbufu,”amesema Mwendak.

Amesema kupitia huduma hiyo kwa sasa wameanza  na walipa kodi 158  ambapo kati ya hapo  wamiliki binafsi wapo 111 wote wameshaitwa  kueleshwa kuhusu huduma hiyo,huduma pia itagusa viongozi wa mihimili mitatu ambapo kwa sasa viongozi 47 kutoka ngazi za juu,”amesema Mwenda.

Akitoa  sababu zakuwahudumia makundi hayo amesema  wamiliki binafsi wa kampuni mchango wao ni mkubwa sana kwa sababu wameanzisha kampuni,wameajiri watu wakati viongozi  wamepewa kipaumbele hicho kwa sababu wana mchangi mkubwa wana majukumu mengi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *