‘WATOTO WENYE UTINDIO WANA HAKI SAWA KAMA WENGINE’

Na Aziza Masoud,Dar es Salaam 

JAMII imetakiwa kutokuwaficha watoto wenye utindio wa ubongo kwani ni watoto kama walivyo wengine na kwamba kufanya hivyo kunazidi  kuwaongezea unyonge zaidi.

Wito huo umetolewa na Doreen Fitzpatrick ambaye ni Mtanzania anayeishi Marekani na Mkurugenzi wa Sassyfly Luxury Event wakati akitoa msaada katika Kituo cha kulelea watoto wenye Utindio wa Ubongo cha Dorcas Homecare Initiative kilichopo Madale, jijini Dar es Salaam.

Akikabidhi msaada huo ambao ni viti saba vya walemavu (wheelchair), diapers pamoja na vyakula mbalimbali, Doreen amesema ameamua kuja Tanzania ili kurudisha shukrani kwa jamii.

“Watoto wenye mtindio wa Ubongo ni watoto kama watoto wengine hivyo wazazi wasiwafiche watoto hao bali wawapeleke katika vituo maalum ili wafundishwe stadi mbalimbali za maisha.

Alisema wazazi wanashindwa kujua kuwa watoto Hawa wanaweza kupata elimu kama watoto wengine na kwamba  wana upeo wa akili na upendo kuliko kitu kingine.

“Nimekuwa nje ya nchi kwa miaka 10, kwahiyo nimerudi Tanzania kurudisha kwa jamii yangu. Na katika kufikiria kitu cha kufanya nikaona ni bora niwasaidia watoto hawa…tunajua kuna vituo vya watoto yatima lakini sio wengi wanajua kuhusu utindio wa Ubongo,” amesema Doreen.

Akipokea msaada huo, Rehema Semfukwe amemshukuru Doreen  kwa kuona umuhimu wa kuwasaidia kwani unaonyesha moyo wa upendo kwa watoto hao wenye mahitaji maalum.

“Tunamshukuru Doreen kwa msaada huu mkubwa, na tunaomba wengine nao wajitokeze waweze kutusapoti katika mambo mbalimbali ikiwemo kupata usafiri wa kuwachukua watoto majumbani mwao kuwaleta hapa kituoni na kuwarudisha,” amesema Rehema.

Alisema Kituo hicho kina jumla ya watoto 15 na wengi wao wanatokea eneo hilo la Madale ambapo asilimia 99 hawawezi kufanya chochote ikiwemo kutembea na kuongea.

“Mungu ametupa maono haya ya kuanzisha Dorcas Homecare Initiative baada ya mimi kupata mtoto mwenye utindio wa ubongo. Kwahiyo kutokana na nimemlea mtoto wa aina hii na kuona changamoto ambazo nimekutana nazo na nikaweza kujua ni kwa namna gani wazazi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *