Maandalizi muongozo mpya wa elimu yapamba moto

*Shule 96 za sekondari zasajiliwa kutoa mafunzo ya amali

Na Mwandishi Wetu,Dar es Salaam

Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia imesema hakuna mwanafunzi atakayeshindwa kujiunga na sekondari kwa sababu ya ufinyu wa miundombinu ifikapo mwaka 2028 kwakuwa imeshafanya maandalizi ya kupokea wanafunzi wa mikondo miwili ambao watamalizia elimu ya msingi mwaka 2027.

Wanafunzi hao ambao ni wale wanaotarajia kumaliza elimu ya msingi kupitia mtaala mpya ambao wataishia darasa la sita pamoja na watakaomalizia darasa la saba mwaka huo ambao kwa sasa wapo darasa la nne.

Akizungumza katika kikao kazi na wahariri pamoja na Waziri wa Elimu Profesa Adolph Mkenda,Mkurugenzi wa Sera na Mipango Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Atupele Mwambene alisema miongoni mwa vitu ambavyo wamezingatia wakati wakutekeleza muongozo mpya wa utoaji elimu ni kuandaa miundombinu ya msingi ambayo itawezesha kutekeleza mwongozo huo.

“Kama mnavyoona utekelezaji wa sera hii ya elimu kwa upande wa umalizaji wa elimu ya msingi inaenda mpaka 2028 ndo wanafunzi wanaanza kuishia darasa la sita lakini wakati huo huo kutakuwa na wale wa darasa la saba nao watakuwa wanamaliza.

“Lengo lakuweka utekelezaji huu mwaka 2028 ni pamoja na kutoa muda kwa serikali kuandaa miundombinu ya msingi ikiwemo madarasa,walimu,vitabu hivyo ifikapo muda huo hakuna mwanafunzi ambaye atashindwa kuendelea na masomo,”alisema Mwambene.

Alisema wanafunzi hao watakaoanza kidato cha kwanza wataanza na mitaala ya mafunzo ya amali pamoja na jumla.

“Wanafunzi watakaofundisha masomo ya jumla watajikita zaidi katika mambo ya kitaaluma huku wale watakaofundishwa masomo ya amali watasoma zaidi mambo ya ujuzi kuanzia kidato cha kwanza hadi cha nne,”alisema Mwambene.

Kwa upande wa Profesa Mkenda akifungua mafunzo hayo alisema serikali imejipanfa vizuri hasa katika mitaala ya mafunzo ya amali ambapo kabla ya utekelezaji wake wameenda katika nchi tofauti tofauti wanazofanya mambo hayo kuchukua ujuzi.

“Huu mtaala wa mafunzo ya amali ni hiyari,hakuna mtu atakayelazimisha,kabla ya mwanafunzi kupelekwa kutakuwa na makubaliano baina ya mzazi na wanafunzi na walimu,lengo letu watu wamalize elimu ya msingi wakuwa na ujuzi,”alisema Profesa Mkenda.

Alisema serikali imeshafanya uchunguzi na kujiridhisha shule zote ambazo zinataka kutoa mafunzo ya amali kama zinakidhi vigezo vinavyohitajika kutoa elimu hiyo.

“Kulingana na vigezo tulivyoviweka shule 96 zimepitishwa kufundisha masomo ya amali Tanzania Bara,kati ya hizo 28 ni za serikali na 68 ni za binafsi,”alisema Profesa Mkenda.

One thought on “Maandalizi muongozo mpya wa elimu yapamba moto

  1. Βeyond ϳust improving grades, primary math tuition nurtures ɑ positive and enthusiastic attitude
    tⲟward mathematics, reducing anxiety ᴡhile igniting genuine іnterest
    in numbeгs and patterns.

    In Singapore’ѕ rigorous secondary education landscape, math tuition Ьecomes indispensable fοr students tо
    deeeply master challenging topics including advanced algebra, geometry, trigonometry, aand statistics tһat serve аs tһe backbone fⲟr О-Level achievement.

    In Singapore’s intensely demanding JC landscape, Η2 Math tuition proves indispensable f᧐r students to confidently conquer advanced
    topics ѕuch aѕ calculus, probability, аnd statistical methods
    tһat carry ѕignificant weight in А-Level papers.

    Online math tuition stands оut for primary students іn Singapore ԝhose parents wɑnt steady
    MOE-aligned practice without fixed centre timings, ѕignificantly
    lowering pressure while building strong foundational numeracy.

    OMT’ѕ flexible understanding tools personalize tһе trip,
    turning mathematics іnto ɑ beloved friend ɑnd motivating steadfast examination dedication.

    Join ᧐ur small-gгoup on-site classes іn Singapore fߋr tailored guidance in ɑ nurturing environment that builds strong foundational math skills.

    Withh trainees іn Singapore Ьeginning official mathematics education fгom tһe first
    day аnd facing hіgh-stakes assessments, math tuition оffers the extra edge required to accomplish tоp performance іn thіѕ crucial subject.

    Math tuition іn primary school bridges gaps іn classroom learning, making sure students comprehend
    complicated topics ѕuch as geometry аnd data analysis
    ƅefore thе PSLE.

    Detailed feedback from tuition instructors ⲟn technique attempts assists secondary trainees gain fгom blunders,
    boosting accuracy foг the real O Levels.

    Junior college tuition supplies accessibility tߋ extra sources ⅼike
    worksheets аnd video descriptions, strengthening Ꭺ Level syllabus coverage.

    Inevitably,OMT’ѕ special proprietary curriculum
    matches tһe Singapore MOE educational program Ьy cultivating independent thinkers equipped fօr
    long-lasting mathematical success.

    Ꭲһe self-paced е-learning ѕystem from OMT is super versatile lor, mаking it simpler to
    manage school and tuition for hiցher math marks.

    Tuition programs іn Singapore offer simulated tests under timed conditions,
    mimicing genuine examination circumstances fߋr
    enhanced performance.

    My web blog: Singapore A levels Math Tuition

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *