Na Mwandishi Wetu,Dar es Saam
MWENYEKITI wa chama cha Mawakala Wanaowatafutia watanzania Kazzi nje ya nchi (TRAA) Bara Abdalla Harid Mohamed amewataka madereva kuchangamkia fursa za nafasi za ajira 1150 za udereva nchini Qatar ambapo jumla ya madereva 900 wanategemewa kutoka Tanzania Bara.
Akizungumza na waandishi wa habari jijink Dar es Salaam Mohamed ambaye pia ni Mkurugenzi wa kampuni inajishugjilisna na masuala ya usafiri Al-Maha Travel alisema kuwa nafasi hizo za ajira wahusika wataenda kwa ajili yakuendesha magari ya mwendokasi yaliyopo nchini humo.
“Kuna nafasi za ajira nchini Qatar zipo 1150 zilizotafutwa na serikali,nafasi hizi ni mara ya pili kutolewa ya kwanza ilikuwa 2025 kati ya watu 800 walienda 500,sasa zimekuja nafasi za madereva ya mwendokasi,usahili itaanza tarehe Februari 9 wanatagemewa watu 900 kutoka Tanzania Bara huku wengine 250 wanatarajiwa kutoka Zanzibar watu 250 ,”alisema.

Alisema usahili wa kazi hiyo ni bure na unatarajiwa kufanyika kwa siku tatu mfululizo ambapo kila siku kutakuwa na usahili wa watu 300.
“Interview (usahili) utakuwa unafanyika kwa watu 300 kwa siku moja ambapo zitakuwa siku tatu,wanotaka kushirikiana waje lakini kwa sharti la mtu kutokuchukua chochote kutoka kwa mfanyakazi ,usahili bure lakini vipimo kama afya unalipia kwakuwa wameelekeza vyeti vitoke kwenue hospitali maalum ikiwemo Aga Khan.

“Tunawaasa watanzania wajitokeze kwa wingi kujisajili kupitia kampuni za Maha Travel,kutakuwa na usahili wa awali kati ya tarehe 4 na 5 katika Chuo Cha Usafirishaji (NIT)kuleta watalaam katika usahili,watu wanatakiwa wajiandikishe wasiopungua 3000 ili kupata idadi inayohitajika,mshahara ni zaidi ya dola 700 anbapo muhusika awapo kazi kulala bure,matibabu na kula bure,”alisema.
Alisema sifa za dereva anayepaswa kufanya usahili wa nafasi hiyo ni kuwa na leseni ya daraja C na E pamoja na kuwa na hati za kusafiria na wasiokuwa nazo watanyiwa utaratibu wakuzipata.


