Na Mwandishi Wetu,Dar es Salaam
MWANASIASA na mbunge wa zamani wa Nyamagana mkoani Mwanza, Ezekia Wenje amesema vijana wana wajibu wa kulinda nchi bila kujali itikadi za vyama vya siasa.
Amesema hayo leo , Jumamosi Mei 16,2026 katika kongamano la wanafunzi wa vyuo lenye kauli mbiu ‘never again’ tuipende, tuitunze , tuilinde nchi yetu’ lililofanyika ukumbi wa Ubungo Plaza jijini Dar es Salaam na kuandaliwa na TAHLISO mkoani hapa.
Wenje amesema kwa takwimu zilizopo vijana nd ndio wengi na mchango mkubwa katika Taifa na ndio watu wanaouweza kuamua hatima ya nchi.

” Kuna tofauti kati ya Serikali na Taifa Kuna tofauti kati ya nchi na Serikali, duniani hapa Serikali zinapita, chukua mfano Marekani kuna wakati Democratic kinaongoza, wakati mwingine Republican, lakini msingi lazima Taifa libaki,” amesema Wenje na kuongeza kuwa;
” Tunaposema never again, tunafanya marejesho kilichotokea Oktoba 29,2025, ndio maama nasema kuna utofauti kati ya nchi na Serikali.


