Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko leo ameshiriki mashindano ya Rombo Marathon yaliyohusisha mbio za Kilometa tano, kumi na 21 na kupongeza waandaaji kwa ubunifu wao uliopelekea marathon hiyo kuendelea kuimarika kila mwaka ambapo licha ya kulenga katika kuimarisha afya kwa washiriki, imejikita katika kuchangia uboreshaji wa huduma mbalimbali za kijamii na utunzaji wa mazingira.
Dkt. Biteko ametoa pongezi hizo tarehe 23 Desemba, 2023 wilayani Rombo mkoani Kilimanjaro, akiwa ni mgeni rasmi katika marathon hiyo ambapo alikimbia kwa umbali wa kilometa Tano akiambatana viongozi mbalimbali wa Kitaifa, Mkoa na Wilaya.