MAKAMU MWENYEKITI UVCCM, SOMBI KUZINDUA WIKI YA VIJANA WA CCM

Na Mwandishi Wetu,Rukwa

Makamu Mwenyekiti wa UVCCM, Ndugu Rehema Sombi Omary (MNEC) atazindua Wiki ya Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) leo tarehe 08 Oktoba 2026 wilayani Kalambo mkoani Rukwa.

Wiki ya UVCCM itakayozinduliwa leo na kuendelea hadi Oktoba 14 inalenga kuwakutanisha Vijana wa nchi nzima sehemu moja kupeana fursa, kubadilishana uzoefu, kujadili mustakabali wa taifa lao Tanzania na kufanyika kwa shughuli mbalimbali zinazogusa jamii pamoja na kuongeza wanachama wapya wa Chama cha Mapinduzi.

Aidha uzinduzi huo unaenda sambamba na maandalizi kuelekea miaka 50 ya kuzaliwa kwa Chama cha Mapinduzi.