Na Mwandisbi Wetu,Rukwa
Ikiwa ni sehemu ya shughuli za Wiki ya UVCCM 2026, Makamu Mwenyekiti wa UVCCM Taifa, Ndg. Rehema Sombi Omary (MNEC), ametembelea Kikundi cha Ukombozi wa Vijana wilayani Kalambo, Rukwa, kinachojihusisha na utengenezaji wa sofa, viti, meza, vitanda na fanicha nyingine.
Kikundi hicho cha Vijana kilichonufaika na mkopo kutoka Halmashauri ya Kalambo, uliotumika kununua vifaa vya kisasa, kuboresha karakana na kuongeza mtaji wa kuendesha shughuli zao.

Ndg. Rehema Sombi amewapongeza vijana hao kwa kutumia fursa za kiuchumi zinazotolewa na Serikali na kuwataka kuendelea kuzitumia kwa ajili ya kujikwamua kiuchumi.

Ziara hiyo ni sehemu ya Wiki ya UVCCM 2026.
kaulimbiu “Mazingira tofauti, fursa sawa kwa vijana,” inayolenga kuwakutanisha vijana, kusikiliza changamoto zao na kuhamasisha matumizi ya fursa zilizopo kwa ajili ya maendeleo.



