Mchinjita autaka umakamu mwenyekiti ACT- Wazalendo

Mwenyekiti wa Chama cha ACT Wazalendo Mkoa wa Lindi, Isihaka Mchinjita amesema anatarajia kugombea nafasi ya Makamu Mwenyekiti wa chama hicho upande wa Tanzania Bara.

Kwa sasa nafasi hiyo kwa upande wa Tanzania Bara inashikiliwa na Doroth Semi ambaye ameitumikia kwa kiwango cha kuridhisha.

Mchinjita, ametangaza nia hiyo mkoani Lindi ambapo ameweka wazi baada ya kuwa Mwenyekiti wa mkoa wa Lindi kwa miaka mitano anaona kwa sasa anafaa kugombea ngazi ya taifa.

“Nimekuwa Mwenyekiti wa Mkoa wa Lindi katika kipindi cha miaka mitano kuanzia mwaka 2019 mpaka sasa na Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama cha ACT Wazalendo. Nimetoa mchango wangu wa ujenzi wa chama chetu katika nafasi hizi mbili kwa uaminifu na moyo wa dhati kwa chama changu.

Ninawashukuru wanachama wenzangu wa Mkoa wa Lindi ambao waliniamini na wajumbe wa Halmashauri Kuu ambao walinichagua kuwa Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *