TTCL YAAHIDI KUENDELEA KUTOA HUDUMA BORA

Na Mwandishi Wetu,Dar es Salaam

SHIRIKA la Mawasiliano Tanzania (TTCL) limeahidi kuendelea kutoa huduma bora kwa wateja wake zenye ubora wa hali ya juu pamoja na kuendelea kusikiliza maoni ya wateja ili kuboresha huduma zao.

Akizungumza leo Oktoba 10, 2025 jijini Dar es Salaam katika kilele cha maadhimisho ya wiki ya huduma kwa wateja Kaimu Mkurugenzi  wa Biashara wa TTCL Humphrey  Ngowi alisema siku ya huduma kwa wateja imeacha alama ya kudumu  katika shirika hilo kwakuendelea kudumisha imekuwa fursa yakukusanya mrejesho  kutoka kwa wateja,kutambua mapungufu na kuandaa maboresho yanayolenga kukidhi mahuraji halisi ya wateja.

“TTCL itaendelea kutoa huduma bora za mawasiliano,tutaendelea kusikiliza maoni  ya wateja wetu,kuboresha huduma zetu na kuhakikisha kila mteja anapata thamani stahiki ya huduma anazostahili,”alisema Ngowi.

Alisema wanapofunga wiki ya huduma kwa wateja  2025 na kauli mbiyu ya ‘Mission Possible’ shirika limewashukuru wateja wote kwa michango yao ,moyo wa ushirikiano na juhudi zao zisizochoka.

Awali Mkurugenzi wa Biashara wa Mkoa wa Dar es Salaam wa shirika hilo Diwani Mwamengo alisema katika katika kipindi chote cha wiki ya huduma kwa wateja shirika limepata fursa yakutathimini mafanikio yao.

“TTCL tutaendelea kutoa huduma bora zakuaminika na kuendelea kusikiliza maoni ya wateja wetu,nawapongeza wateja wetu kwakutuunga mkono  na tunawasisitiza wengine watuunge mkono ili waweze  kukuza uchumi wa kidigitali  kama ilivyo sasa,”alisema Mwamengo.

Naye mmoja wa wateja wa kampuni hiyo Petro Njau aliwataka wananchi kutumia huduma za kampuni hiyo kwakuwa ina kasi na nafuu.

“Mimi TTCL natumia kuanzia nyumbani,natumia binafsi nyumbani na pia natumia kwenye kampuni sifa ya intaneti hii ipo kasi na bei zake za kizalendo kwa maisha yetu ukiwa na mtandao ambao bei zipo chini ila kasi ya ajabu unaweza kufanya kazi,kikubwa tuendelee kutumia na kusapoti vya kwetu,”alisema Njau.