WAKULIMA WAFUGAJI WAITWA BANDA LA TRA NANE NANE

Na Mwandishi Wetu,Dodoma

MAMLAKA ya Mapato Tanzania (TRA) imewataka wakulima na wafugaji  kufika katika banda hilo ili kuweza kupata elimu ya kodi hasa katika Mfumo wa  Jumuishi wa Kodi za Ndani (IDRAS)   pamoja na kupatiwa  namba ya mlipa kodi (TIN) bure.

Akizungumza katika maonesho  ya wakulima  nchini yanayofanyika katika viwanja vya Nzuguni mjini Dodoma, Afisa Mwandamizi wa kodi wa TRA, Jacqulime  Rutale  alisema  katika banda hilo kuna maafisa wa mamlaka hiyo ambao wanatoa elimu ya kodi   kwa wananchi hasa katka mfumo huo jumuishi wa IDRAS.

“Tupo hapa  kwa ajili ya kuwahudumia wananchi sasa ni wakulima wafugaji na wafanyabiashara tupo kwa ajili ya kutoa elimu ya kodi inayohusiana na maswala mbalimbali kimfumo ikiwemo mfumo IDRAS pamoja na huduma ambazo tunazitoa katika maonyesho haya ya Nanenane,”alisema 

Alisema katika maonesho hayo pia tuna tini na makadirio kwa maana wateja wakija ambao hawana TIN watapatiwa TIN na kufanyiwa makadirio .

Alisema lakini pia kuna mawakala wa TRA  kwa ajili ya kuwahudumia watu ambao wanahitaji mashine za kiekitroniki  (EFDs) kwa wananchi pamoja na nembo za stempu za kodi.

Alisema  wanatoa pia huduma ya elimu nemba za vinywaji  kwa maana  pamoja vivutio vya misamaha ya kodi katika eneo la ufugaji na uvuvi.

“Nipende  kuwakaribisha wananchi wote kwa ujumla kufika kwenye banda letu la mamlaka ya mapato Tanzania ambapo tuko kwenye jengo la Financial Institution ama taasisi za fedha tunapatikana hapo karibuni wananchi wote wakulima wote tuko kwa ajili ya kuwahudumia,”alisema.

 Naye   Shabani Pazi mkazi wa Dodoma ambaye ni mmoja wa wateja  alisema amefika bandani hapo kwa ajili ya kupata huduma ya namba ya utambulisho wa biashara  ambapo  alikuwa anapata changamoto ya kimfumo katika kufanya maombi.

“Nimekuja hapa ndani ya muda mfupi nimepokelewa nimehudumiwa kwa wakati, kwa hiyo haikuwa shida sana kwa hiyo wale ambao wanahitaji huduma za TRA  tuwaambie  wapo ndani ya Dodoma basi wafike kwenye banda la TRA a hapa katika maonesho ya Nane Nane watahudumiwa vizuri tu kwa mujibu wa mahitaji yao,”alisema ..