TANESCO YAWAPA ONYO WANANCHI WANAOIBA,KUCHOMA MOTO MIUNDOMBINU YA UMEME NJOMBE NA IRINGA 

Na Mwandishi Wetu,Njombe

SHIRIKA la Umeme Tanzania (TANESCO) limetoa onyo kwa wananchi wa mikoa ya Iringa na Njombe wanaofanya uharibifu wa miundombinu ya umeme ikiwemo kuchoma nguzo na kusisitiza kuwa itawachukulia hatua kali zakisheria.

 Taarifa kwa umma  iliyotolewa na Tanesco imeeleza kuwa kitendo cha kuchoma moto miundombinu ya umeme kimeleta hasara kubwa ambapo taarifa  inaonyesha kuwa mpaka sasa jumla nguzo 66, na moto unaendelea kuwaka.

Kati ya nguzo hizo kwa.mkoa wa Njombe jumla ni Nguzo (39) zimechomwa ambapo Mgala(13), Utengule(3), Iboya (2),Image (2), Igoma (2), Utalingolo(4), Yakobi (13)]. 

Katika  wilaya ya Makete jumla nguzo (27) ambapo Ikonda(16), Ilela(5), Ipelele (3) na Lupila (3)