Na Mwandishi Wetu,Dar es Salaam
MAMLAKA ya Usafiri wa Anga Tanzania(TCAA) imetumia Siku ya Kimataifa ya Usafiri wa Anga Duniani(ICAD) kushiriki katika mbio za Marathon zilizoandaliwa na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM).
Mbio hizo zilizoongozwa na Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dkt. Dotto Biteko, zilihudhuriwa pia na Rais mstaafu wa awamu ya nne Jakaya Kikwete .
Maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Usafiri wa Anga Duniani (ICAD) ambayo kilele chake ni Desemba 7,2024 hufanyika kila mwaka duniani.
Maadhimisho yameenda sambamba na kutimia kwa miaka 80 tangu siku hii ilipoanza kuadhimishwa mnamo Desemba 7 mwaka 1944.
Watumishi wa TCAA licha ya kufanya kazi zao za ki udhibiti na kuongoza ndege pia hushiriki katika michezo mbalimbali ikiwa ni hatua ya kuweka afya katika hali bora wakati wote.
Mbali na marathon TCAA pia imefanya shughuli mbalimbali wiki iliyopita ikiwemo kutoa elimu na kuhimiza wanafunzi wa sekondari kusoma masuala ya anga.