Na Mwandishi Wetu,Geita
Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa na Mlezi wa CCM Mkoa wa Geita, Rajab Abdallah, amewasili mkoani Geita na kupokelewa na mamia ya wananchi waliojitokeza kwa wingi kumpokea.
Rajab Abdallah, ambaye pia ni Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Tanga, amewasili mkoani humo leo, Novemba 5, 2026, ambapo msafara wake umeanzia katika Hoteli ya Lenny na kuelekea Ofisi za CCM Mkoa wa Geita.

Katika mapokezi hayo, viongozi mbalimbali wa chama na Serikali walikuwepo, akiwemo Mbunge wa Geita Mjini, Mhandisi Chacha Mwita Wambura, Katibu wa CCM Mkoa wa Geita, Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (MNEC) Mkoa wa Geita, Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Geita, pamoja na wanachama na vijana waendesha bodaboda.
Wananchi na wanachama wa CCM walijitokeza kwa wingi kushiriki
mapokezi hayo yaliyofanyika katika Mkoa wa Geita.



