TTCL :KIPINDI CHA KUJIENDESHA KWA HASARA KIMEKWISHA

Na Aziza Masoud,Dar es Salaam

MKURUGENZI Mkuu wa Shirika  la Maawasiliano Tanzania (TTCL)  Moremi Marwa amesema  wamefanya mabadiliko makubwa yakimfumo  ili waweze kutengeneza faida  zaidi kupitia huduma wanazozitoa hivyo  kwa sasa kipindi cha kutengeneza hasara kimekwisha na sasa wanajiendesha kisasa zaidi.

Marwa ametoa kauli hiyo leo Juni 4, 2026 alipotembelea banda la TTCL katika viwanja vya Maonesho ya Biashara 50 Dar es Salaam(DTIF)  maarufu kama Sabasaba,amesema  katika matukio kadhaa ya hivi karibuni wameonyesha ni jinsi gani shirika hilo  linaendelea kufanya mabadiliko ili kuweza kujiendesha kibiashara na kutengeneza faida.

Alisema utekelezaji huo ni maelekezo ya Rais Dk.Samia Suluhu Hassan ambayo aliwapatia karibu miaka miwili iliyopita na kwamba walikuwa  wanafanya  mabadiliko ili shirika hilo lisonge mbele.

“Lengo letu lilikuwa shirika lijiendesha kisasa kwakufanya biashara lakini vile vile kutengeneza faida kwa hiyo kwa mwaka uliopita huu wa mwaka 2025/2025 tulitengeneza faida karibu Sh Sh bilioni 23 na kama ambavyo muulize swali amesema mwaka huu pia wa 2025/26 ambao kimsingi tumemaliza juzi tukiangalia kilichopo tayari lakini siwezi kutaja kwakuwa bado havijakaguliwa ni mpaka vikikaguliwa na sisi  ndio tunaweza kusema.

 “Lakini tayari kwamba mapato yanaendelea kuongezeka na tunategemea vile vile faida iweze kuongezeka tukilinganisha na mwaka uliopita kwa hivyo ni shirika ambalo linazidi kwenda mbele tukikuza mapato yetu tukiongoza wateja tulionao lakini vile vile tukiendelea kutengeneza faida tunahisi kwamba kile kipindi cha utengenezaji wa hasara kimekwisha na sasa hivi shirika linajiendesha kisasa ikihudumia wateja wetu lakini katika kufanya hivyo tutengeneze mapato kwa kutumia mapato vizuri katika kutengeneza faida,”alisema Marwa.

Mbali na hilo Marwa pia alizumgumzia bidhaa mpya zilizoletwa mwaka huu katia maonesho hayo na TTCL ikiwemo intaneti ya kasi ya juu ya Supersonic Speed, kituo cha FTTX Experience Center kinachoonesha matumizi ya teknolojia ya nyumba janja (Smart Home), pamoja na huduma za cloud computing kupitia Kituo cha Taifa cha Kuhifadhi Data (NIDC).

“Uchumi wa kidijitali hauwezi kufikiwa bila kuwa na mawasiliano ya uhakika na intaneti yenye kasi. Ndiyo maana tunaendelea kutumia Mkongo wa Taifa kuleta huduma bora n8a za gharama nafuu kwa Watanzania,” alisema CPA Marwa.

Alifafanua kuwa teknolojia hizo zinawezesha matumizi mbalimbali ya kidijitali ikiwemo mifumo ya usalama wa nyumba, matumizi ya vifaa vya nyumbani kwa njia ya mtandao, michezo ya mtandaoni na huduma za video zenye ubora wa juu.