TPHPA YAZINDUA TEKNOLOJIA MPYA YA KUBAINI VISUMBUFU VINAVYOATHIRI UZALISHAJI WA MAZAO
Na Asha Mwakyonde, Dodoma MAMLAKA ya Afya ya Mimea na Viuatilifu Tanzania (TPHPA), imezindua matumizi ya teknolojia mpya ya vipimo vya vinasaba (DNA) kwa ajili ya kubaini visumbufu mbalimbali vinavyoathiri uzalishaji wa mazao nchini, ikiwemo magonjwa na wadudu waharibifu. Tanzania imekuwa nchi ya kwanza duniani kuingiza teknolojia hiyo katika sekta ya kilimo. Hayo yamesemwa leo,…

