Na Mwandishi Wetu,Dar es Salaam
SPIKA wa Bunge Mstaafu Anne Makinda amewapongeza Wakala wa Umeme Vijijini (REA) kwakupiga hatua kubwa yakuwasaidia wananchi kupitia ubunifu wao wakusambaza umeme vijijini pamoja na nishati safi ya kupikia na kwamba wametoa unafuu wa maisha kwa wananchi hasa wa vijini.
Makinda alitoa kauli hiyo alipotembelea katika banda la REA waliopo katika Maonesho ya 50 ya Biashara Dar es Salaam yanayofanyika katika Viwanja vya Malimu Nyerere maarufu kama Sabasaba,alisema nishati safi ya kupikia ni muhimu kwa wananchi wote nchini kwani itapunguza athari zitokanazo na matumizi ya nishati isiyo safi na kupelekea Magonjwa kwa watumiaji.

“REA wamepiga hatua kubwa katika kusambaza umeme Vijijini na kutumia ubunifu ambao haukuwepo,miaka ya nyuma huduma za umeme vijijini ilikuwa hazipatikani kwa urahisi,pia uanzishwaji wa vya mafuta vijijini ni njia mojawapo yakusaidia wananchi kuingia katika matumizi ya nishati safi,”alisema Makinda.
Alisema ametembelea katika banda hilo na kuona baadhi ya bidhaa za REA zilizopo katika banda hilp zinatumiwa vijijini na kwamba baadhi ya teknolojia zilizopo sio zile zakubadilika ghafla.

Alisema matumizi ya nishati mbadala hasa vijijini imeongezeka hasa kupitia kampeni ya Rais Samia Suluhu Hassan ya matumimi ya nishati hiyo ambapo aliwataka REA kutumia majukwaa kama ya mikutano yakisiasa vijijini kuelimisha matumizi ya nishati hiyo.



