Na Mwandishi Wetu, Dodoma
SHULE ya Sekondari Itega ya jijini Dodoma imeibuka mshindi wa mashindano ya usalama barabarani yaliyoandaliwa kwa udhamini wa kampuni ya TotalEnergies Marketing Tanzania, na kujinyakulia zawadi ya Sh milioni 15.
Itega imewashinda shule za sekondari Wella na Dodoma zilizokuwa zikichuana katika mashindano hayo yaliyolenga kuongeza uelewa wa wanafunzi kuhusu sheria na kanuni za usalama barabarani.
Fedha hizo zitatumika kuboresha mazingira ya usalama barabarani katika shule hiyo, ikiwa ni sehemu ya juhudi za kuwajengea wanafunzi uelewa na utamaduni wa kuzingatia matumizi sahihi ya barabara.

Akizungumza katika hafla ya kukabidhi zawadi hizo, Afisa Taaluma wa Mkoa wa Dodoma, Justin Machela, amewataka wanafunzi walioshiriki mashindano hayo kuwa mabalozi wa usalama barabarani kwa kueneza elimu waliyoipata kwa wenzao na jamii inayowazunguka.
Machela amesema elimu hiyo inapaswa kuonekana katika vitendo, akiwataka wanafunzi kuwa mfano wa kuzingatia sheria za barabarani, kutambua maeneo hatarishi na kutoa taarifa kwa walimu pamoja na mamlaka zinazohusika.

Pia amewahimiza kushirikiana na Jeshi la Polisi katika kuhamasisha usalama barabarani, huku wakizingatia usalama wao na kuepuka kujiweka katika mazingira hatarishi.
Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Sheria wa TotalEnergies Marketing Tanzania Limited, Marsha Msuya, amesema tangu kuanzishwa kwa mashindano hayo mwaka 2022, kampuni hiyo imetumia zaidi ya Sh milioni 400 kuratibu na kutekeleza programu hiyo nchini.
Amesema mashindano hayo hayalengi kutangaza washindi pekee, bali kuwajengea wanafunzi uwezo wa kutambua changamoto za usalama barabarani katika mazingira yao na kubuni njia za kukabiliana nazo.
Ameeleza kuwa kupitia programu hiyo, wanafunzi hupatiwa mafunzo ya usalama barabarani na kushirikishwa katika kuchunguza mazingira ya shule zao ili kubaini vihatarishi vinavyoweza kusababisha ajali na kupendekeza hatua za kuviondoa.

Naye Sajenti Ester Makali kutoka Dawati la Elimu kwa Umma la Kikosi cha Usalama Barabarani, amesisitiza umuhimu wa kuendelea kutoa elimu hiyo kwa wanafunzi na jamii kwa ujumla ili kujenga uelewa mpana kuhusu wajibu wa kila mmoja katika kuzuia ajali.
Kwa upande wake, Nancy Augustino Mathias, balozi wa usalama barabarani kutoka Shule ya Sekondari Itega, amesema wanafunzi wamejipanga kutumia elimu waliyoipata kuhamasisha wenzao na jamii kuzingatia sheria za barabarani.
Ushindi huo unaifanya Itega kupata nafasi ya kuiwakilisha Tanzania katika mashindano ya kikanda yatakayoshirikisha nchi mbalimbali, zikiwemo Uganda, Madagascar na Ivory Coast.
Mshindi wa mashindano hayo ya kikanda atapata nafasi ya kushiriki mashindano ya dunia.