Na Mwandishi Wetu,Rukwa
Makamu Mwenyekiti wa UVCCM Taifa, Ndg. Rehema Sombi Omary (MNEC), amezindua rasmi Wiki ya UVCCM 2026 katika Wilaya ya Kalambo, Rukwa, akisisitiza vijana kukutana, kusikilizana, kubaini fursa na kuzigeuza changamoto kuwa fursa za maendeleo.
Ametembelea miradi ya vijana wanaonufaika na mikopo ya asilimia 10 ya Halmashauri na kuzungumza na vijana pamoja na wananchi wa Kalambo. Pia ametoa salamu za Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, akisisitiza dhamira yake ya kuhakikisha vijana wanapata fursa sawa za maendeleo.

Amesema kaulimbiu ya Wiki ya UVCCM 2026, “Mazingira tofauti, fursa sawa kwa vijana,” inawahimiza vijana kutumia fursa zilizopo katika maeneo yao, huku akiwataka kuenzi tunu za Taifa, kuongeza wanachama wapya na kutekeleza wajibu wa kulipa ada za uanachama.
Wiki ya UVCCM 2026 inaanza leo, tarehe 8 Oktoba, na itaendelea hadi Oktoba 14, 2026.Kaulimbiu: Mazingira tofauti, fursa sawa kwa vijana



