WANANCHI WAFURIKA SABASABA KUSHUHUDIA MAONESHO YA BIASHARA

Na Mwandishi Wetu,Dar es Salaam

WANANCHI wamejitokeza kwa wingi katika Viwanja vya Sabasaba jijini Dar es Salaam leo Julao 7, 2026 kushiriki na kutembelea Maonesho ya Kimataifa ya Biashara yanayoendelea kuvutia washiriki kutoka ndani na nje ya nchi.
Tangu asubuhi, viwanja hivyo vilishuhudia msongamano mkubwa wa wageni waliokuwa wakitembelea mabanda mbalimbali ya taasisi za umma, kampuni binafsi na wajasiriamali, wakijionea bidhaa, huduma na ubunifu unaoonyeshwa katika maonesho hayo.


Baadhi ya wananchi walisema maonesho hayo yamekuwa fursa muhimu ya kupata taarifa kuhusu bidhaa na huduma mpya, kujifunza teknolojia mbalimbali pamoja na kuanzisha mahusiano ya kibiashara.


Kwa upande wao, waandaaji wa maonesho wameeleza kuridhishwa na mwitikio mkubwa wa wananchi, wakisema idadi ya wageni imeendelea kuongezeka siku hadi siku.

Wamewahimiza wananchi kuendelea kutembelea maonesho hayo ili kujifunza, kufanya biashara na kuunga mkono bidhaa zinazozalishwa nchini.


Maonesho ya Sabasaba hufanyika kila mwaka na hukutanisha washiriki kutoka sekta mbalimbali za uchumi, yakilenga kukuza biashara, uwekezaji, ubunifu na maendeleo ya viwanda nchini.