WANANCHI WAFURIKA KUSHUHUDIA  UZINDUZI WA KITUO CHA KIHISTORIA CHA JNHPP

Na Mwandishi Wetu, Rufiji

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Samia Suluhu Hassan, leo Agosti 22, 2026 anatarajiwa kuzindua rasmi Kituo cha Kuzalisha Umeme cha Julius Nyerere (JNHPP), kilichopo Rufiji, Mkoa wa Pwani.

Kutokana na umuhimu wa kituo hicho hasa katika kuendelea kuchechemu sekta ya nishati nchini  kwakupata umeme wa uhakika viongozi mbalimbali kutoka nje na ndani ya nchi pamoja wananchi wa eneo la Rifiji na maeneo ya jirani wamefurika  ili kushuhudia uzinduzi huo wa wakihistoria.

Kituo hicho chenye uwezo wa kuzalisha megawati 2,115 kinatajwa kuwa hatua kubwa katika kuongeza uwezo wa Tanzania kuzalisha umeme na kuimarisha upatikanaji wa nishati ya uhakika kwa shughuli za kiuchumi na kijamii.

Uzinduzi huo ni tukio la kihistoria katika safari ya Tanzania ya kujenga mfumo wa nishati unaoaminika, huku ukitarajiwa kuchochea uzalishaji, uwekezaji na ukuaji wa uchumi.

Kwa mujibu wa Serikali, mradi huo umegharimu takribani Sh7.452 trilioni, fedha zilizotolewa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Mradi huo pia umetajwa kuwa mkubwa zaidi wa kuzalisha umeme kuwahi kutekelezwa nchini kwa kutumia fedha za ndani.

Mpaka sasa mradi huo umeshakamilika na mitambo yote tisa kuanza kufanya kazi, hatua iliyowezesha kituo kuanza kuongeza kiwango cha umeme kinachoingizwa katika Gridi ya Taifa.

Taarifa ya Wizara ya Nishati inaonyesha kuwa hadi Mei 31, 2026, JNHPP ilikuwa imechangia takribani asilimia 44.9 ya umeme wote uliozalishwa na kuingizwa kwenye Gridi ya Taifa katika kipindi cha mwaka uliotangulia.

Mradi huo ulianza kujengwa rasmi Juni 2019 na unatekelezwa katika Mto Rufiji. Mbali na uzalishaji mkubwa wa umeme, kituo hicho kimeundwa pia kwa malengo ya kudhibiti mafuriko na kuhakikisha mtiririko wa maji unaodhibitiwa katika mazingira.

Uzinduzi wa leo unafanyika baada ya hatua mbalimbali za utekelezaji wa mradi huo, ukiwamo uzinduzi wa ujazaji maji katika bwawa mwaka 2022 na kukamilika rasmi kwa mradi mwaka 2025.

Kwa Serikali, kukamilika na kuanza kufanya kazi kwa kituo hicho kunatarajiwa kuongeza uhakika wa umeme, kupunguza changamoto za upungufu wa uzalishaji na kuweka mazingira bora kwa shughuli za viwanda, biashara na uwekezaji nchini.

Kuhusu kituo hicho

 Wazo la kujenga kituo hicho lilitolewa  miaka ya 1970 na Hayati Mwalimu Julius Nyerere ambapo serikali yake ilifanya tafiti mbalimbali za kitalaam na upembuzi yakinifu  ili kubaino uwezekano wa kujenga  bwawa na kitup kikubwa cha kuzalisha umeme  katika eneo la Stiegler’s Gorge.

 Eneo hilo lilitambuliwa kuwa na uwezo mkubwa wa kuzalisha umeme kutokana na rasilimali kubwa ya maji katika bonde la Rufiji.

Mradi huo ulilenga kuongeza uzalishaji wa umeme nchini na kuchangia kudhibiti mafuriko  katika maeneo ya Kibiti na Rufiji,hata hivyo changamoto za kiuchumi na ukosefu wa fedha zilichelewesha utekelezaji wake.

Pamoja na changamoto lakini bado viongozi walioingia madarakani baada ya Mwalimi Nyerere walikuwa wakifanya jitihada mbalimbali zikiwemo kufanya tafiti mbalimbali ili kuhakikisha ujenzi huo unafanyika  bila kuathiri maisha ya watu waliozungukwa na mrafi huo.

Katika uongozi wa serikali ya awamu ya Tano iliyoongozwa na Hayati Fk.John Magufuli  ndiye aliyefanya uamuzi huo wa kihistoria na kudhubutu kuanza ujenzi huo ambapo   alisaini mkataba na kampuni ya JV AC-EE  ya Misri  kwa ajili ya ujenzi wa mradi huo.

Ujenzi ulianza rasmi Julai 28 ,2019 chini ya Hayati Dk.Magufuli ambapo mpaka anafariki Machi 2021 ujenzi huo ulikuwa umefikia asilimia 33.

Kutokana na umuhimu wa mradi huo Rais Dk.Samia baada yakuingia madarakani  ilipofika Desemba  mwaka 2021 aliuendeleza mradi huo kwa kasi kubwa  na kumalizia asilimja 67.7 zilizobaki.