MAENEO YALIOATHIRIWA NA MVUA BARABARA YA DAR-LINDI-MTWARA YOTE NI SHWARI
Barabara ya Dar es salam-Lindi-Mtwara sasa imerejea katika hali ya kupitika baada ya kukamilika urejeshaji…
Na Mwandishi Wetu,Dar es Salaam MAMLAKA ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) imefanikiwa kukamata jumla ya kilogramu 1,983.31 za dawa mbalimbali za kulevya, kilogramu 3,012.5 na lita 17,960 za kemikali bashirifu, vidonge 286 na chupa 1,001 za dawa tiba zenye asili ya kulevya katika kipindi cha mwezi Machi 2026. Aidha katika ukamataji…
Na Mwandishi Wetu,Dar es Salaam VIJANA wakitanzania wametakiwa kushiriki kutoa mawazo bunifu yenye lengo la kutoa suluhisho ya mambo yanayoikabili jamii ambapo mshindi wa wazo hilo atapewa zawadi ya Sh Milioni 50. Hayo yamesemwa jijini Dar es Salaam juzi na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-Maendeleo ya Vijana, Joel Nanauka wakati akiwatangazia vijana kushiriki Shindano…
Na Mwandishi Wetu,Dar es Salaam TANZANIA imeingiza vipengele 41 katika Tuzo za Utalii na Usafirishaji Duniani (World Travel Awards), hatua hiyo inaimarisha nafasi yake na kukua zaidi katika sekta ya ya utalii na kuwa kinara barani Afrika Akizungumza leo Aprili 11,2026 jijini Dar es Salaam, Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano wa Bodi ya Utalii Tanzania…
Na Mwandishi Wetu Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Shirikisho la Urusi, tarehe 03 Aprili 2026, zimesaini hati ya makubaliano ya ushirikiano katika sekta ya uchukuzi, ikiwa ni hatua muhimu ya kuimarisha maendeleo ya miundombinu na kubadilishana uzoefu wa kitaalamu kati ya nchi hizo mbili. Makubaliano hayo yalisainiwa pembezoni mwa Mkutano…
Durban, Afrika Kusini.Naibu Waziri Wa Uchukuz Mheshimiwa David Kihenzile, amesema ziara ya mafunzo katika Bandari ya jiji la Durban imempa uzoefu mpana kuhusu namna uwekezaji wa kimkakati unavyoweza kuongeza ufanisi wa bandari. Akizungumza baada ya kutembelea bandari hiyo yenye takribani gati 58 zinazohudumia mizigo, magari na abiria Naibu Waziri Kihenzile amesema uwekezaji mkubwa katika miundombinu…
Na Aziza Masoud,Dar es Salaam KAMPUNI ya Izze Ride imezindua mfumo mpya wa usafiri mtandaoni ambao unalenga kuleta mapinduzi katika sekta ya usafirishaji pamoja na kuwainua kiuchumi madereva watakaofanya kazi na mfumo huo. Akizungumza jana Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Izze Ride Fredrick William, alisema ujio wa mfumo huo mpya wa usafiri wa kidijitali unapenga …
Na Mwandishi Wetu,Zanzibar KAMISHNA Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bw. Yusuph Juma Mwenda amesema Mamlaka hiyo itaanzisha utaratibu mpya wa kuingiza mafuta ya kupikia Tanzania Bara kutoka Zanzibar ili kuwezesha kufanyika kwa biashara halali ya mafuta hayo na kuzuia mafuta ya magendo kuingizwa nchini. Akizungumza na wafanyabiashara wanaoagiza mafuta ya kupikia nje ya…
Na Mwandishi Wetu,Dar es Salaam BENKI ya Biashara Tanzania (TCB) imezindua kampeni maalum ya Nina Ndoto nayolenga kuwawezesha Watanzania kufikia ndoto zao kwa kuwapatia suluhisho sahihi za kifedha, hatua inayotarajiwa kuchochea ukuaji wa uchumi na kuongeza ustawi wa jamii. Kampeni hiyo inalenga kuimarisha upatikanaji wa huduma za kifedha kwa makundi mbalimbali ya wananchi, hususan wajasiriamali,…
Na Mwandishi Wetu,Dodoma SERIKALI kupitia Tume ya Madini imeendelea kusisitiza utekelezaji wa sheria na kanuni katika sekta ya madini, ikiwataka wamiliki wa leseni kuhakikisha shughuli za uchimbaji zinawanufaisha watanzania na kulinda maslahi ya taifa. Akizungumza jijini Dodoma kwenye kikao cha wamiliki wa leseni, Kamishna wa Tume ya Madini, Mhandisi Theonestina Mwasha, amesema kipaumbele cha Serikali…
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) zimefanya kikao cha pamoja cha wataalam wa sekta ya uchukuzi leo tarehe 18 Machi, 2026 Mkoani Kigoma, chenye lengo la kuharakisha utekelezaji wa miradi ya kimkakati ya usafiri na kukuza biashara kati ya nchi hizo mbili. Ujumbe wa Tanzania katika kikao…