WAMILIKI WA VYOMBO VYA MOTO WAHIMIZWA KUKATA BIMA 

Na Aziza Masous,Dar es Salaam

KAMPUNI  ya NIC Insurance imewahimiza wamiliki wa vyombo vya moto nchini kuhakikisha wanakata bima ili kujikinga na athari ambazo zitawasababishia hasara zinazoweza kujitokeza pindi yanapotokea majanga au ajali.

Akizungumza katika Maonesho ya 50 ya Biashara Dar es Salaam  Sabasaba,Afisa Bima wa NIC Insurance, Iman  Mollel  bima katika vyombo vya moto ni muhimu  kukata bima ili kuweza kuepuka hasara mbalimbali.

“Miongoni mwa bima  tulizonazo ni  pamoja  na bima ya vyombo vya moto,tunatoa bima kwa vyombo hivi,sisi kwa upande wa vyombo vya moto pindi mtu apatapato shida inayohusu bima  anahudumiwa ndani ya muda mfupi,sisi huwa hatuna mlolongo mrefu muhusika akipata shida analeta nyaraka zake anapata stahiki zake ,”alisema Mollel.

Alisema NIC pia  imeendelea kuboresha utoaji wa huduma kwa kuhakikisha madai ya fidia kwa magari yaliyoharibika kiasi cha kutotengenezeka (total loss) yanashughulikiwa kwa haraka, ambapo malipo hufanyika ndani ya siku saba baada ya mteja kukamilisha nyaraka zote zinazohitajika.

Alisema bima za vyombo vya moto vinavyotolewa na NIC ni pamoja na  magari binafsi, magari ya biashara, magari ya mizigo, mabasi na magari ya abiria, bajaji pamoja na pikipiki, ili kuhakikisha wamiliki wake wanapata kinga dhidi ya hasara zinazoweza kujitokeza.

Alisema  NIC imeweka  utaratibu wakuhudumia wateja wao kidigitali ambapo wateja wanaweza kupata huduma za bima kwa njia ya mtandao, hatua inayolenga kupunguza gharama na muda wa kusafiri kufuata huduma katika ofisi za kampuni hiyo.

Mollel amewataka wananchi wanaotembelea Maonesho ya Sabasaba kufika katika banda la NIC Insurance ili kupata elimu kuhusu huduma mbalimbali za bima pamoja na ushauri wa kitaalamu utakaowasaidia kuchagua bima zinazokidhi mahitaji yao.