MFUMO WA GHALA PROJECT UTAONGEZA UWAZI KWA MKULIMA
Na Aziza Masoud, Dodoma CHUO Kikuu Cha Dodoma (UDOM) kimetengeneza mfumo wa kidijitali wa Ghala Project unaolenga kuongeza uwazi katika matumizi ya mfumo wa stakabadhi ghalani na kuwawezesha wakulima kupata taarifa za mazao yao kwa wakati. Mfumo huo unaotekelezwa kupitia Ghala Project, unalenga kutatua changamoto zinazowakabili wakulima katika kupata taarifa baada ya kuwasilisha mazao yao maghalani,…

